Na Luppy Kung’alo wa Jeshi la Polisi Dodoma
Picha mbalimbali za Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Bw. David Misime akitembelea wilaya ya Mpwapwa na vijiji vyake kwa ajili ya kuhamasisha mkakati wa Polisi Jamii na uanzishaji wa vikundi vya ulinzi shirikishi katika vijiji na kata za wilaya ya mpwapwa hivi karibuni.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Bw. David Misime akiachana na gari lake na kuungana na kikundi cha ulinzi shirikishi kilichofahamika kwa jina la Mwananzele kilichopo katika kijiji cha Mbori kata ya Matomondo wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, waliokwenda kumpokea akiwa njiani kabla ya kufika kijijini hapo kwa ajili ya kuongea na wanakijiji hao masuala mbalimbali yahusuyo ulinzi na usalama wa watu na mali zao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Bw. David Misime, akifanya Ukaguzi kwa askari wa kikundi cha ulinzi shirikishi cha Mwananzele cha kijiji cha Mbori kata ya Matomondo wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, kuangalia na kujua ukakamavu wao uko imara kiasi gani.
Wazee wa Kimila wa Kijiji cha Mbori katika kata ya Matomondo wilayani Mpwapwa, wakimvika vazi rasmi na kumkabidhi mkuki Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Bw. David Misime Kama ishara ya kumtambua rasmi kuwa kamanda na mlezi wa kikundi cha ulinzi shirikishi cha mwananzele katika kata hiyo.
Wanakijiji wa Mbori katika Kata ya Matomondo Wilayani Mpwapwa wakimsikiliza kwa makini Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Bw. David Misime, ambaye alikuwa akiwahutubia wanakijiji hao kuhusu miradi mbalimbali Iliyopo katika mpango wa Polisi jamii na Ulinzi shirikishi juu ya umuhimu na faida zake kwa jamii hiyo.