SSRA, MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII NA NIDA imekutana ili kujadili jinsi vitambulisho vya Taifa vinavyoweza kutumika ili kuongeza wigo wa Wanachama katika Sekta ya Hifadhi ya Jamii na hivyo kupunguza umaskini Nchini .
Pichani kushoto mwakilishi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) akitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Bi. Irene Isaka, Mkuu wa Tehama SSRA Dr. Carina Wangwe na Wakurugenzi, Mameneja na maofisa wa Tehama wa mifuko ya hifadhi ya Jamii jinsi vitambulisho vya taifa vinavyoweza kusaidia katika kupanua wigo wa hifadhi ya Jamii kwa kila Mtanzania.