Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115280

KWIECO WAFANYA MKUTANO MKUU MKOANI KILIMANJARO

$
0
0
Wajumbe wa mkutano mkuu wa shirika lisilo la kiserikali linaloshughulika na maswala ya jinsia na wanawake mkoani Kilimanjaro, (KWIECO) wakifanya sala kabla ya kuanza kwa mkutano mku wa shirika hilo.
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali linaloshughulika na maswala ya jinsia na wanawake mkoani Kilimanjaro, (KWIECO) Clement Kwayu akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa shirika hilo.
Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali linaloshughulika na maswala ya jinsia na wanawake mkoani Kilimanjaro, (KWIECO) Elizabeth Minde akizungumza wakati wa mkutano huo.
Wajumbe wa mkutano mkuu wa KWIECO.

Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi

JUMLA ya wateja 1,660, wamepatiwa ushauri nasaha wa kisheriauliotolewa na shirika lisilo la kiserikali linaloshughulika na maswala yajinsia na wanawake mkoani Kilimanjaro, (KWIECO), katika mwaka 2012.

Hayo yameelezwa na mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo Bi Elizabeth Minde, wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika makao mapya ya shirika hilo yaliyopo eneo la Shanty town mjini Moshi.

Amesema katika kipindi hicho kambi nne za msaada wa kisheria ziliwekwa na ushauri wa kisheria ulitolewa na kuwashirikisha jumla ya watu 1,020 huku kesi muhimu 62 kati ya 50 zilizopendekezwa zikifunguliwa mahakamani katika kuongeza upatikanaji wa haki za wanawake na watoto.

“Katika kuongeza uelewa na ushiriki wa jamii katika kulinda haki za Binadamu na jinsia, kamati za haki za Binadamu ziliundwa katika ngazi za vijiji katika kata saba za Mkoa wa Kilimanjaro, ambapo mafunzo ya uongozi yalitolewa kwa viongozi wa serikali za mitaa wapatao 318 hivyo kuwajengea ujasiri katika kushughulikia masuala ya kijinsia na haki za watoto”, alisema. Minde

Aidha Minde aliendelea kusema kuwa katika kuongeza uelewa, kulinda na kutetea haki za watoto, mafunzo ya haki za watoto yalitolewa kwa wajumbe 65, wanafunzi 960 na walimu 150, ambapo kamati saba za haki za watoto na klabu 42 za watoto ziliundwa mashuleni.

Aliendelea kusema kuwa katika kuwajengea uwezo wa kiuchumi, jumla ya wanawake 63 walioko maeneo ya pembezoni, walipewa misaada ya kujiajiri wenyewe na 43 walipewa misaada kwenye ajira zisizo rasmi.

Minde alisema katika kipindi hicho cha mwaka jana, kiwango cha umasikini miongoni mwa walengwa wa shirika hilo kilikuwa bado ni changamoto kubwa, sambamba na ile ya watoto kutokuwa na uwezo wa kuchangia mawazo yao mbele ya wazazi jambo ambalo alisema husababishwa na tamaduni na imani potofu za kimila.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115280

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>