Dar es Salaam ni moja ya majiji ambayo yanakua kwa kasi kiuchumi. Hii ni kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu, uwekezaji, Viwanda nk. Haya yote yamekuwa yanachangia kwa sehemu kubwa ongezeko la uhitaji wa maji na inakadiriwa kuwa kwa miaka 15 ijayo uhitaji utaongezeka mara mbili zaidi.
Inakadiriwa kuwa zadi ya asilimia 50 ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam hawajafikiwa na huduma ya maji ya bomba. Matumizi ya maji ya kisima kwa jijini Dar es Salaam ni tatizo kutokana na uchafuzi wa mazingira utokanao na Viwanda, maji taka na taka za wakazi wa jiji hilo.
Hii sasa yawezekana ikawa neema kwa wakazi wa jiji hilo kwa ushirikiano huu uliongiwa baina ya Wizara ya Maji na Idara ya Maji ya hapa Hamburg, Ujerumani iitwayo Hamburg Wasser . Ushirikiano huu utalenga kusaidia tatizo la maji katika jiji hili la Dar es Salaam
Kutoka kushoto ni : Eng. Christopher Sayi ( Katibu mkuu Wizara ya Maji ), Godfrey Matola, Mh. Prof. Jumanne Maghembe ( Waziri wa Maji ) , Reinhard Paulsen , Ully Mbuluko, Moses Haule, Eng. Christian Gunner ( Kutoka Hamburg Wasser ) , Mh. Christopher Mvula ( Kaimu Balozi wa Tanzania Ujerumani ) na Godwin Msigwa . Wakipiga picha ya pamoja baada ya Hotuba kutolewa na Waziri wa maji Tanzania na pia kutoka upande wa wenyeji Hamburg Wasser.
Prof. Jumanne Maghembe ( Waziri wa maji ) akisisitiza jambo kwa Petra Hammelman ( Balozi wa Heshima wa Jamhuri ya Tanzania – Hamburg ) baada ya kutoa Hotuba ndani ya jengo la Seneti Hamburg .