Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

CHAJA YA READYSET KUTOA NJIA MBADALA YA CHANZO CHA NISHATI.

$
0
0
 Meneja Mauzo wa Vodacom Tanzania, kupitia mradi wa"Readyset Charge" Bw. Nicholaus Kizenga,akiwaonesha wakazi wa Ubungo jijini Dar es Salaam jinsi yakutumia chaji hiyo inayotumia  mionzi ya jua,zinazopatikana katika maduka ya Vodacom nchini na  zinatumika kwa ajili ya kuchajia simu za mkononi na matumizi mbalimbali ya kibiashara,kwa wajasiriamali  wadogowadogo ,Elimu hiyo ilifanywa na kampuni ya Fenix International kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania.
 Mfanyabiashara wa Ubungo jijini Dar es Salaam Rashid Ally(katikati)akimsikiliza Meneja Mauzo wa Vodacom Tanzania, kupitia mradi wa"Readyset Charge" Bw. Nicholaus Kizenga(kulia)akimuelimisha namna ya kutumia chaji inayotumia  mionzi ya jua,Chaji hizo zinazopatikana katika maduka ya Vodacom nchini na  zinatumika kwa ajili ya kuchajia simu za mkononi na matumizi mbalimbali ya kibiashara,kwa wajasiriamali  wadogowadogo hapa nchini,Elimu hiyo ilifanywa na kampuni ya Fenix International kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania.
 Mfanyabiashara wa Ubungo jijini Dar es Salaam Rashid Ally(katikati)akionyeshwa jinsi ya kuchaji simu na Meneja Mauzo wa Vodacom Tanzania, kupitia mradi wa"Readyset Charge" Bw. Nicholaus Kizenga(kulia)kwa kutumia chaji inayotumia  mionzi ya jua, zinazopatikana katika maduka ya Vodacom nchini na  zinatumika kwa ajili ya kuchajia simu za mkononi na matumizi mbalimbali ya kibiashara,kwa wajasiriamali  wadogowadogo hapa nchini.Elimu hiyo ilifanywa na kampuni ya Fenix International kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania.
======   =========   =======

Ikiwa ni asilimia 18.4% ya Watanzania wanaotumia nishati ya umeme, Watanzania sasa wamebadilika na kuanza kutumia njia mbadala ya vyanzo vya nishati. Takribani asilimia 90 ya Watanzania wanatumia nishati ya kuni, na asilimia 8 wakiwa wanatumia mafuta ya taa.

Njia mbadala ya vyanzo vya nishati hapa nchini Tanzania zina adhari kubwa kwa jamii husika zikiwa ni pamoja na uharibifu wa mazingira na afya. Mfano mzuri ni matumizi ya kuni yanayochochea sana ukataji wa miti, na nishati itokanayo na petroli kama mafuta ya taa zikipelekea uchafuzi wa hali ya hewa, kitu kinachopelekea madhara kwa binadamu na mazingira kwa ujumla.

Kwa kulizungumzia hili, inatakiwa chanzo cha nishati ambacho kitakuwa rafiki wa mazingira na rahisi kupatikana hapa nchini. Makampuni ya kitaifa na kimataifa yanatakiwa kuja na ujuzi mpya na kuweka mawazo pamoja ili kupata ubunifu ambao lengo lake siyo kutoa nishati peke yake, mbali na kupatia Watanzania walioko vijijini na mijini kipato.

Aidha kampuni ya mawasiliano ya Vodacom, mwaka huu mwezi wa 4 kwa kushirikiana na Fenix International, walizindua bunifu ambayo lengo lake siyo upatikanaji wa nishati tuu mbali na kupatia Watanzania ajira.
Makampuni haya mawili alizindua ReadySet, chaja ambayo inatumia nishati ya jua na kuchaji simu na vifaa vingine ambavyo huwa vinachajiwa.

Katika uzinduzi huo, ilifahamika kuwa takribani watumiaji million 600 wa mitandao ya simu hutumia trillion 16 za Kitanzania kwa mwaka kusafiri kwenda kuchaji simu zao na nishati ya umeme wa betri za magari
Kwa uanzilishi wa chaja za Readyset, Watanzania wengi wanaoishi vijijini sasa wanaweza kutumia simu kwa ajili ya mawasiliano kuwasiliana na wawapendao bila kusafiri umbali mrefu na kutumia hela nyingi za nauli.

Akiongea huku akionyesha kifaa hicho jijni Dar es Salaam wiki hii, meneja wa kampuni ya mawasiliano ya simu ya Vodacom, Nicholus Kizenga, alielezea kuwa Watanzania wamekuwa wakisubiria jambo hili kwa mda mrefu.
"Chaja hizi zimezinduliwa wakati muafaka kabisa hapa nchini kwasababu zitaleta msaada mkubwa sana kwa Watanzania walio wengi kwa kuwa zitawasaidia kutunza mali kama pesa na muda," alisema Kizenga.
Pia, Kizenga aliendelea kusema kuwa chaja hizi zimeleta suluhisho la kupunguza gharama na nishati kwakuwa zinaweza kuchaji simu kumi kwa wakati mmoja, taa za ndani, radio, na kompyuta.

Kifaa hicho kinagharimu laki tatu na ishirini (320,000) na kinaweza kikamuingizia mtu anayefanya biashara ya kuchajisha simu shilingi 64,000 kwa mwezi. Hili litawasaidia kujiwekea takribani dola kumi za kimarekani kwa kutokutumia mafuta ya taa.

Alihimiza Watanzania wasiogope kutumia kifaa hicho kwasababu kinaendana na mazingira ya Kitanzania na kinapopata shida kuna mafundi wa kuvitengeneza kwasababu kina warantii  Maneno Mashaka, mmoja wa watu waliokuwepo wakati wa maonyesho hayo, alisema ana matumaini kwamba kwa maendeleo haya, Tanzania inakuwa kiuchumi bila kuwa na gharama kubwa kama za kufungiwa umeme, na kuingiza mafuta yatokanayo na petroli nchini.

"Huu ni uzinduzi mkubwa sana, na wengi wetu ambao tulikuwa hatuna umeme majumbani mwetu tumelazimika kutumia mkaa na mafuta ya taa. Haya yametuletea athari kubwa sana za kiafya. Kwa  kutumia chaja hizi tunaweza kuingiza kipato na wakati huo huo kupata nishati ya umeme,"alisema Mashaka

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>