Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Magavana kutoka nchi za Afrika Mashariki na nchi majirani zao wakutana jijini Arusha

$
0
0
Mahmoud Ahmad Arusha.
 
Magavana kutoka nchi za Afrika Mashariki na nchi majirani zao wamekutana jijini hapa katika mkutano wao wa 13 pamoja na mengine kujadili mtangamano wa kuwa na sarafu moja ya bara la Afrika kwa kuanzia na kuwa na mtangamano wa sarafu za kikanda.

Akizungumza kwenye mkutano huo Gavana wa Tanzania Beno Ndulu alisema kuwa kuna chama cha mkutano huu ujulikanao kama (CENTRAL BANK OF AFRICA SUMMIT) na kuwa mkutano huo ni wa 13 unaowakutanisha magavana na manaibu gavana kutoka kwenye wanachama wa chama hicho.

Akazitaja nchi wanachama wa jumuiya hiyo kuwa  ni nchi za jumuiya ya Afrika mashariki na majirani zao nchi za congo drc,Ethiopia, Sudan, Komoro,Mauritius,na Ghana mada kuu ya mkutano huo ikiwa ni kujenga mtangamano wa sarafu ya pamoja kwa kuanzia na ukanda na baadae Afrika nzima.

Gavana Ndulu alisema kuwa baada ya mawazo ya wakuu wa nchi wanachama wa AU kupitisha maadhimio yao ya kutaka kuwa na sarafu za pamoja hivyo wao kama wadau wa sekta ya fedha wanakutana kujadili mtangamano huo.

“Tunajiangalia tutafikaje huko na je tumejiandaaje kufika huko hili ndio lengo la kukutana hapa leo kwani timu hii ndiyo inadhamana ya kutufikisha huko”alisema ndulu

Mkutano huo wa siku tatu unaowashirikisha wadau wa fedha kutoka kwenye nchi za afrika  ulinza tangia juzi na kufunguliwa leo jijini hapa na Gavana Ndulu

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>