Na Abdulaziz,Lindi.
Wajumbe kutoka kata 21 za wilaya kilwa mkoani Lindi waliounda baraza
la katiba la wilaya nusura wazipige kufuatia mvutano kuhusu nafsi ya
waziri mkuu kwenye serikali ya shirikisho katika katiba ijayo.
Tukio hilo lilitokea baada ya mwenyekiti wa kundi la sita la tume prof
Palamagamba Kabudi lilipokuwa wilayani kilwa ambapo walichangia
kutokana na makundi yalioanishwa.
Katika makundi hayo yalipewa hoja kujadili ambapo kundi na moja
lilipewa hoja ya maadili lingine mihimili ya dola pamoja na , haki za
binadamu na suala la uwepo wa Muungano,
Akichangia maoni yake kwenye kundi lilokuwa likijadili suala la
Maadili,bw Shaibu mohamedi Nginji alieleza kuwa uwepo wa serikali ya
shirikisho hakuna umuhimu wa kuwa na waziri mkuu kwa kuwa majukumu
yake yatafanywa na makamu wa rais.
“hakuna haja ya kuwa na waziri mkuu kwani kufanya hivyo ni sawa na
kurudi kwenye muungano wa serikali mbili,jambo ambalo aliwezi
kukubalika kwa kuwa hakuna sababu ya kuogopa muundo wa serikali tatu
na ndio utakuwa ukombozi wetu watu wa bara.
Hoja hiyo ilipingwa na wajumbe wengine wa kundi liloongozwa na Haji
Ibrahimu na kusababisha kurushiana maneno na wajumbe wengine kususia
mjadala na kuwaachia wachache wakiendelea kujadili .
Mvutano huo ulipata ufumbuzi baada ya mwenyekiti wa kundi la sita la
tume Prof Paramaganda Kabudi kuwataka wajumbe hao kutambua kuwa kila mjumbe aliekuwepo kwenye kikao hicho ana haki ya kuchangia mawazo yake ili mradi havunji sheria za Nchi na kufanya hivyo ndio maana ya
kuunda katiba ya Wananchi baada ya kutoa maoni yao