Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Waendesha BodaBoda Nyangao Lindi wakabidhiwa leseni Baada ya kuhitimu Mafunzo

$
0
0
Na Abdulaziz Video,Lindi

Vijana 38 wa kijiji cha Nyangao B tarafa ya Mtama ktk halmashauri ya wilaya ya Lindi, wamepongezwa kwa kwa uamuzi wao wa kujiunga na kuanzisha kikundi cha bodaboda kwa lengo la kulinda mali zao wenyewe kupitia dhana ya ulinzi shirikishi na polisi jamii.

Pongezi hizo zimetolewa na Afisa Mnadhimu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi, Kamishina Msaidizi wa Polisi Renatha Mzinga kwenye hafla fupi ya kukabidhi leseni za udereva wa bodaboda na vitambulisho vya polisi jamii kwa vijana 18 iliyofanyika ktk uwanja wa kituo cha polisi kijijini hapo.

Katika risala yao,vijana hao wamerishukuru jeshi la polisi ktk tarafa hiyo likiongozwa na Afisa wa polisi jamii wa tarafa ya Mtama Peter Msafiri kwa juhudi kubwa za kupambana na wimbi la wizi wa uvunjaji wa maduka na majumbani na kuahidi kusaidiana kulisambaratisha wimbi hilo.

Naye mwenyekiti wa kikundi hicho cha bodaboda Ally Manjolo, ametoa wito kwa abiria wanaotumia bodaboda kuanzia sasa kukagua vitambulisho na leseni za madereva waliohitimu mafunzo ya udareva na sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali zisizo na msingi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>