Picha na habari naa Dixon Busagaga
wa Globu ya Jamii,Moshi
MTU mmoja ambaye jina lake halijafahamika mara moja amefariki Dunia huku wengine sita wakijeruhiwa vibaya kufuatia ajali mbaya iliyotokea juzi usiku majira ya saa moja katika eneo la Kawawa wilayani Moshi.
Majeruhi wa ajali hiyo walikimbizwa katika hosptali ya rufaa ya KCMC muda mchache baada ya kutokea kwa ajali hiyo iliyohusisha magari mawili likiwemo basi la abiria lijulikanalo kwa jina la Metro ambayo yaligongana uso kwa uso na Loli aina ya Fuso lililokuwa likielekea Dar es salaam. Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo ilitokea baada ya dereva wa gari aina ya Fuso kujaribu kulipita Loli jingine aina ya Scania likiwa na trela lake kabla ya kukutana na basi la Metro lililokuwa likitokea Dar es salaam kuelekea Arusha ndipo magari hayo yakagongana uso kwa uso.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz alithibitsha kutokea kwa ajali hiyo huku akitaja namba za usajili wa magari yalihusika katika ajali hiyo kuwa ni basi la Metro aina ya Yutong lenye namba za usajili T 129 BQL likiendeshwa na Oscar na Fuso lenye namba za usajili T 615 AWB lililokuwa likiendeshwa na Goodluck Aseri.(45)lilikuwa likitokea Moshi kuelekea Njia panda Himo.
Kamanda Boaz alisema Dereva wa basi aliyefahamika kwa jina moja la Oscar alifariki dunia papo hapo huku kondakta na abiria wengie watano katika basi hilo walipata matibabu katika hosptali ya rufaa ya KCMC.
Alisema jeshi la polisi mkoa wa Kilimanjaro linamshikilia Dereva wa Fuso kwa maelezo zaidi na kwamba mara uchunguzi utakapokuwa umekamilika atafikishwa mahakamani kwa mujibu wa sheria za usalama Barabarani.
Muonekano wa mbele wa gari aina ya Fuso baada ya kugongana uso kwa uso na basi a Metro baada ya kile kilichosemekana kuwa ni kupata hitilafu katika mfumo wa breki.
Gari aina ya Fuso ikipakia mizigo iliyokuwa katika gari lililopata ajali baada ya kugongana uso kwa uso na basi la Metro na kusababisha kifo cha mtu mmoja.
Sehemu ya mabaki ya gari aina ya Fuso.
Dereva wa Fuso aliyefahamika kwa jina la Goodluck Aseri akiwa amelazwa katika hospitali ya KCMC akiwa na pingu mkononi.