Taasisi kilele ya TAHA inayoundwa na wakulima wanaojishughulisha na kilimo cha 'horticulture' nchini Tanzania hatimaye imefungua rasmi ofisi zake kuu katika visiwa vyenye marashi ya karafuu Zanzibar. Ufunguzi wa ofisi hizo zilizo mtaa wa Kikwajuni kwenye Jengo la mfuko wa barabara ulitanguliwa na ziara fupi ya kutembelea maeneo ambayo Taasisi hiyo imeanzisha mashamba darasa na kusajili vikundi vya wakulima ili waweze kufaidika kwa karibu zaidi na ushauri wa kiufundi katika masuala ya kilimo cha 'horticulture' hali kadhalika masoko ya kuuza bidhaa zao ndani na nje ya nchi. | ||||
Mkurugenzi wa TAHA akiteta Jambo na Mtaalamu wake kwa upande wa Visiwani Mzee Biwi wakati alipotembelea moja ya mashamba ya tikiti maji ya wakulima ambao ni wanachama wa TAHA.
|
↧
TAHA yafungua rasmi ofisi zake za Zanzibar
↧