Ijumaa hii Ankal alitembelea Chuo cha Maafisa wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (Tanzania Military Academy - TMA) huko Monduli, Arusha, na kukutana na baadhi ya wadau wakubwa wa Globu ya Jamii ambao wapo chuoni hapo wakibukua. Ankal alifarijika sana kukuta kuwa hata maafande sio tu ni wafuatiliaji wakubwa wa Libeneke hili bali pia walimshauri aendelee kuheshimu maadili pamoja na sheria na kanuni za taaluma ya habari, ikiwa ni pamoja na kuendelea kuepuka kujeruhi hisia za mtu ama watu, jambo ambalo wametaja kuwa ni moja ya siri za mafanikio haya kiasi yaliyopatikana.
Ankal akiwakumbusha wadau hao wa TMA kuwa Septemba 8, mwaka huu Globu ya Jamii itasherehekea miaka tisa toka izaliwe kule Helsinki, Finland, na akawakaribishwa kwenye sherehe za kukata na shoka ambazo zinaandaliwa. Stay tuned...Libeneke Oye!