Omar Sykes enzi za Uhai wake.
Na Swahili TV
Familia ya mwanafunzi mtanzania aliyeuwa mjini washington DC, marehemu Omary Sykes inatarajiwa kuingia nchini Marekani leo hii, swahili TV inaripoti. Kwa mujibu wa vyanzo vyetu familia hiyo itaongozwa na baba wa marehemu bwana Adamu Sykes na baba mkubwa wake bwana Ilyasa Sykes.
Marehemu ambaye alikuwa na miaka 22, ni mjukuu wa mpigania uhuru maarufu wa Tanzania mzee Kleist Abdulwakili sykes na pia ni ndugu wa msanii star wa bongo Flava Dully Sykes.
Omar aliuawa kwa shambulio la risasi karibu na maeneo ya chuo anachosoma cha Howard University usiku wa alhamisi julai 4, 2013 akiwa na mwenziwe katika mtaa wa Fairmont North West, kwa mujibu wa Polisi Washington DC (MPDC) na Polisi wa chuo hicho (HPD), watu wawili ndio wanaoshukiwa kuhusika na mauaji hayo.Wahusika bado hawajatiwa mbaroni.
Kwa mujibu wa habari za ndani za jeshi hilo la Polisi, kitengo maalum cha uchunguzi wa mauaji kilishaanza upelelezi mkali ukiongozwa na Bwana Gabriel Truby wa MPDC na wameieleza Swahili TV kuwa licha ya upelelezi wanaoendelea nao wanaomba ushirikiano wa wananchi kwa ajili ya kufanikisha uchunguzi wao. Zawadi ya dola za Kimarekani 25,000 itatolewa kwa yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa wauaji hao.
Maripota wa Swahili TV wamefanikiwa kufanya mawasiliano na kitengo cha mauaji cha MPDC, Howard University Police pamoja na familia ya marehemu Omar Sykes. Kwa mujibu wa maelezo yao mwili wa marehemu bado upo hospitalini kwa ajili ya uchunguzi na swahili TV inaahidi kuwaletea habari zote zinazohusiana na upelelezi huu.
Stay tuned kwa exclusive story.
Tembelea http://swahilitv. blogspot.com/
Stay tuned kwa exclusive story.
Tembelea http://swahilitv.