Kaka Michuzi habari ya kazi,
naomba nirushie hii kwa jamii.kundi la Bodaboda Kampen ambalo linajihusisha ya kutoa elimu ya usalama barabarani kwa madeleva wa bodaboda wakishirikiana na jeshi la polisi ambapo mwaka huu wamejitolea kutoa mkono wa pole kwa wagonjwa waliopata ajali za pikipiki,ambapo tulianzia na hospitali ya Taifa Muhimbili na tunatarajia kufanya kila mkoa.
kwa hiyo tunaomba wadau wajitokeze kutupa sapoti katika kutoa elimu kwa waendesha Boda Boda na kuwatembelea mahospitalini pindi wapatapo matatizo kwani mahospitalini wamesahaulika sana wengi wao ndugu zao wapo mbali,kwahiyo wanatakiwa kupata misaada midogomidogo kama nguo, sabuni, mafuta, maji, miswaki, juice, matunda, hiyo ndio misaada tuliotoa jana tarehe 07/07/2013 katika hospitali ya Taifa Muhimbili kitengo cha Mifupa (Moi).
tunaomba wadau wajitokeze kutusapoti tuweze kutembelea katika hospitali za mkoa wa Dar es salaam baada ya hapo mikoani na vijijini.
tunatumai ombi letu litakubaliwa kwa wadau mbalimbali.
Msafara ukielekea Muhimbili.
Tulipokelewa na Uongozi na kutoa tulichofika nacho.
Mmoja wa wahanga wa Boda Boda akizungumza na wanahabari.