Kama ilivyo ada ya kila jumapili kufanya mazoezi ya mbio za pole pole (jogging) pamoja, leo Wanabiafra wamekimbia zaidi ya kilomita nane katika kuadhimisha sikukuu ya saba saba. Mbio hizo zilianza majira ya saa 12:25 asubuhi yalipo makao makuu ya klabu kupitia barabara ya Kawawa hadi Moroko, barabara ya Kibaki hadi kwa Mwalimu Nyerere, barabara ya Rose Garden Hadi Sayansi, brabara ya Maji Machafu na kufuata barabara ya Akachube mpaka Peace Mwananyamala, barabara ya kwa Kopa, barabara ya Dunga hadi Hombus kisha barabara ya Kawawa hadi Msikiti wa Mtambani tukaingia "service road" ya upande Kinondoni Hospital mpaka Manyanya (Chimbinga) ambapo mbio ziliishia. Fuatilia matukio kwa picha mbalimbali!
Maeneo ya kwa Nyerere |
Barabara ya kuelekea Rose Garden. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA |