Mchezaji wa timu ya Flamingo,Jamali Ngoma akicheza pool wakati wa mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya Safari Lager National Pool Championship 2013 mkoa wa Pwani yaliyofanyika kwenye Baa ya Kontena Kibaha Maili moja, kwa kuzikutanisha timu za Flamingo na Ya kwetu.
Mchezaji wa timu ya Flamingo,Syakyala Mwansasu akionyesha kiwango wakati wa mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya Safari Lager National Pool Championship 2013 mkoa wa Pwani yaliyofanyika kwenye Baa ya Kontena Kibaha Maili moja, kwa kuzikutanisha timu za Flamingo na Ya kwetu.
UONGOZI wa chama kipya cha mchezo wa katika mkoa wa Pwani (PWAPA), umewataka wadau wa mchezo huo mkoni humo kuwapa sapota ya kutosha ili uweze kupanda chati kwa haraka kama ilivyo katika mikoa mingine.
Hayo yalisema kwenye ukumbi wa Kontena Kibaha na mwenyekiti wa chama hicho, Sebastian Shembilu wakati alipokuwa akifungua mashindano ya 'Safari Lager National Pool Championship 2013' ngazi ya mikoa ambako yanafanyika kwa mara ya kwanza. Shembilu alisema kuwa nguvu ya pamoja kati ya uongozi na wadau wa mchezo huo mkoani humo ndiyo itakayosaidia kuuinua mchezo huo kwa haraka zaidi.
Alisema kuwa mchezo huo mkoani humo hauna mwamko kama ilivyo katika mikoa mingine kutokana na kwamba wachezaji wengi wanauchukulia kama sehemu ya kupoteza muda.
"Vipaji vya wachezaji wa mchezo wa pool mkoa wa Pwani vipo isipokuwa hauna mwamko kama ilivyo katika mikoa mingine, hivyo niwaombe wadau wa mchezo huo watuunge mkono katika kuupandisha chati kwa haraka ili na wachezaji wanaoucheza waweze kutambua umuhimu wake na kuacha kuuchukulia kama sehemu ya kupoteza muda,"alisema Shembilu.
Aliongeza kuwapongeza wadhamini wa mashindano hayo, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager pamoja na chama cha mchezo huo Tanzania (TAPA) kwa kuuongeza mkoa huo katika mashindano hayo.
"Hatuna budi kuwashukuru wadhamini wa mashindano hayo pamoja na TAPA kwa kukubali kuuongeza mkoa wa Pwani katika kushiriki mashindano hayo ambapo nina imani kuanzia sasa utaanza kupata mwamko,alisema.
Shembilu alisema kuwa jumla ya timu saba zinashiriki mashindano hayo katika ngazi ya mkoa huo ambazo ni Flamingo, Annex, Five Star, Kilivyo 'A', Kilivya 'B', Yakwetu na wenyeji Kontena.