Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115279

WANAFUNZI CHANGAMKIENI OFA YA LAPTOP KUTOKA VODACOM NA MODEM YENYE GB6

$
0
0
Meneja Mauzo ya ziada wa Vodacom Tanzania Liginiku Millinga (kulia) akionesha moja ya kompyuta mpakato (Laptop) wakati wa hafla ya uzinduzi kati ya kampuni ya Red Dot na Vodacom ambapo sasa wateja watanunua laptop za DELL kwa bei nafuu na kupata ofa ya modem bure yenye GB 6 kwa miezi miwili kutoka Vodacom. wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Joseline Kamuhanda na Meneja wa Red dot Tanzania Nishad Mairal.
Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Joseline Kamuhanda na Meneja wa Red dot Tanzania Nishad Mairal,wakimshuhudia Meneja Mauzo ya ziada wa Vodacom Tanzania Liginiku Millinga (kulia) akionesha Modem yenye GB 6 wakati wa hafla ya uzinduzi wa ushirikiano kati ya Red Dot na Vodacom ambayo mteja atakaenunua kompyuta mpakato(laptop)aina ya DELL kwa bei nafuu atapata ofa ya modem hiyo bure kwa muda wa miezi miwili.

Katika kukidhi kasi ya maendeleo ya teknolojia kwa watanzania hususani wanafunzi wa vyuo na watu mbalimbali kampuni ya Vodacom kwa kushirikiana na Intel Tanzania wameungana na kutangaza ofa ya kompyuta mpakato (Laptop) itakayouzwa kwa bei nafuu pamoja na modem iliyounganishwa na intanet kwa miezi miwili.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla iliyofanyika katika banda la Vodacom kwenye maonesho ya 37 ya biashara ya kimataifa Dar es Salaam jana, Meneja wa Malipo ya kabla wa Vodacom Liginiku Milinga alisema kuwa mtu yeyote atakaye nunua kompyuta hiyo atazawadiwa modem yenye ya intanet yenye GB 6.

"Pindi mteja atakaponunua kompyuta hii atapewa modem yenye namba maalum ya Modem ambayo atatakiwa kuituma kwenda Vodacom na ataunganishwa moja kwa moja na huduma ya intanet kwa kupata GB 3 kwa miezi miwili mfurulizo,”

Milinga amesema Vodacom imekuwa mbele katika kuhakikisha inarahisisha maisha ya Watanzania ili kuwawezesha kukidhi mahitaji yao ya kila siku kwa kundana na kasi ya maendeleo ya sayansi na teknolojia.

“Dunia ya sasa imeshuhudia mapinduzi makubwa ya kiteknolojia laptop pamoja na internet vimekuwa vitendea kazi muhimu kwa kila mtu, tumeona vyema kuja na ofa hii ili kuwawezesha watanzania zaidi kuweza kumiliki Laptop kwa bei nafuu,” alisema milinga.

Aidha aliongeza kuwa ni vyema sasa wakati huu wanafunzi wanaotegemea kujiunga na vyuo mwakani kuchangamkia ofa hiyo ili kujiweka mahala pazuri zaidipindi watakapojiunga na vyuo kutokana na uhitji mkubwa wa vitendea kazi hivyo kwa wanafunzi wa vyuo.

Mbali ya hayo mteja atakae nunua kompyuta hizo anapata fursa ya kuingizwa kwenye droo kubwa ya sh.200,000 itakayokuwa ikifanyika mara moja kila mwezi iwapo mteja atatumia huduma ya M-pesa kufanyia manunuzi ya mahitaji mbalimbali.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115279

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>