Pichani ni Muuguzi wa UMATT,Bi.Mery Biseko akionesha namna ya kutumia Kondom za kike kwa vijana mbalimbali (hawpao pichani) waliojitokeza katika tamasha la mafundisho ya afya ya uzazi yanayoendelea katika viwanja vya Kihesa sokoni,mkoani Iringa.
Mratibu wa mradi wa TUWALEE kutoka katika shirika la UMATT,Bi Jemida Kulanga, akitoa elimu ya Afya ya Uzazi kwa vijana mbalimbali waliokuwa wamejitokeza katika tamasha la mafundisho ya afya ya uzazi yanayoendelea katika viwanja vya Kihesa sokoni,mkoani Iringa.
======== ======= =======
Shirika la UMATT linakabiriwa na changamoto ikiwemo ya kutokuaminika katika huduma wanazotoa, hasa katika suala la upimaji afya kwa wateja wao na walio wengi hawana elimu juu ya afya ya uzazi.
Hayo yamesemwa na Mratibu wa mradi wa TUWALEE kutoka katika shirika hilo,Bi Jemida Kulanga, wakati akizungumza na wandishi wa habari katika tamasha la mafundisho ya afya ya uzazi yanayoendelea katika viwanja vya Kihesa sokoni,mkoani Iringa.
Bi.Jemida amesema kuwa kuna haja kubwa ya kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana ambapo itasaidia kupunguza magonjwa mbalimbali yatokanayo na ngono pamoja na mimba zisizotarajiwa .
Amesema kuwa wameamua kufanya tamasha hilo kutokana na asilimia kubwa ya wateja wao waliofika katika ofisi zao ,wameonekana kuwa na uelewa mdogo juu ya afya ya uzazi ikiwemo matumizi ya mpango wa uzazi.
Hata hivyo katika mafunzo hayo pia wameweza kufundisha matumizi ya Kondomu za kike kwa wanawake ,kwani wanawake wengi wameonekana kutokujua matumizi yake na wengine kutokuijua kabisa kondom hiyo ya kike.
Aidha amewataka vijana kutafuta habari zinazohusu afya ya uzazi ili kuepuka magonjwa hatarishi yanayohusiana na suala zima la uzazi.