Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando akiwaonyesha waandishi wa
habari (hawapo pichani) nyumba watakayojishindia washindi wa Airtel
Yatosha Shinda Nyumba 3 iliyozinduliwa leo katika ofisi za Airtel
Morrocco jijini Dar Es Salam ,akifuatiwa na meneja masoko wa Airtel bi
Anethy Muga.
habari (hawapo pichani) nyumba watakayojishindia washindi wa Airtel
Yatosha Shinda Nyumba 3 iliyozinduliwa leo katika ofisi za Airtel
Morrocco jijini Dar Es Salam ,akifuatiwa na meneja masoko wa Airtel bi
Anethy Muga.
Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye uzinduzi wa promosheni ya Airtel Yatosha Shinda Nyumba 3, iliyofanyika katika ofisi za Airtel jijini Dar Es Salam ,akifuatiwa na meneja masoko wa Airtel bi Anethy Muga.
====== ====== ====== ======
Wateja Airtel sasa kujishindia Nyumba 3 za kisasa kupitia huduma ya YATOSHA
* Kila siku mshindi mmoja kuondoka na kitita cha shilingi milioni moja
* Mteja mmoja kujinyakulia nyumba 1 kila mwisho wa mwezi kwa miezi mitatu
Ijumaa Julai 5, 2013 Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania
inayotoa huduma ya mawasiliano bora na nafuu zaidi nchini leo
imezindua promosheni mpya kabambe itakayowawezesha wateja wote wa
Airtel Yatosha kujishindia zawadi mbalimbali huku wakiendelea
kufurahia huduma ya Airtel yatosha ya siku, wiki au mwezi kama
kawaida.
Uzinduzi wa promosheni hiyo mpya ya Airtel Yatosha inadhihirisha
dhamira halisi ya Airtel kupitia huduma yao kabambe ya Airtel Yatosha
yenye lengo la kutoa huduma nafuu huku wakiendelea kuwafaidisha wateja
wao nchi nzima
Akiongea wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo katika ofisi kuu ya
Airtel Tanzania, Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bw, Suni Colaso alisema
"Leo Airtel tunafanya tukio la kihistoria mara baada ya uzinduzi wa
huduma ya Airtel yatosha. Sasa tunawazawadia wateja wetu wa Yatosha
kwa aina ya kipekee kabisa, Kila atakaejiunga na huduma ya Airtel
Yatosha moja kwa moja atakuwa amejihakikishia nafasi ya kujishindia
zawadi ya Nyumba ya kisasa au kitita cha Pesa taslim.
Tutakuwa na mshindi mmoja wa kila siku atakaeibuka na shilingi milioni moja, na kama hiyo haitoshi kila mwisho wa mwezi tutatoa nyumba moja kwa mshindi mmoja kwa muda wa miezi mitatu" .
Nyumba tunazotoa kwa wateja wetu ni za kisasa kabisa ili kudhihirisha
kuwa Airtel Yatosha, ni nyumba yenye vyumba vitatu, sebule pamoja na
jiko, itakuwa ndani ya fance iliyonakishiwa katika hali ya mvuto zaidi
ili kumfanya mshindi wetu kufurahia zaidi kuwa mteja wa Airtel
yatosha", aliongeza kusema Bw Colaso
Akifafanua jinsi ya kushiriki promosheni hiyo Meneja Masoko wa Airtel
Bi Anethy Muga alisema " Ili mteja kushiriki promosheni hii, mteja
atatakiwa kuendelea kujiunga na kutumia huduma yetu ya Airtel Yatosha
ya Kila SIKU, WIKI, au MWEZI kwa kupiga *149*99#, kwa kufanya hivyo
moja kwa moja utakuwa umeingia kwenye nafasi ya droo ya kila siku,
wiki au ya mwezi na unaweza kujishindia zawadi zetu kabambe Ikiwemo
Nyumba.
Promosheni hii ya Airtel Yatosha ni maalum kwa wateja wote wa Airtel
yatosha wa malipo ya kabla, Ikiwa hujajiunga na Airtel jiunge leo na
utumie huduma ya Airtel Yatosha ili upate nafasi ya kujishindia nyumba
ya kisasa kila mwisho wa mwezi au pesa taslimu ndani ya siku tisini
kila siku
Airtel ilizindua huduma ya Airtel Yatosha miezi mitatu iliyopita kwa
lengo la kuwawezesha wateja wake kupata huduma bora na nafuu zaidi,
lengo la huduma hii ni kumpatia mteja huduma nafuu ya sms , muda wa
maongezi pamoja na kufurahia mtandao wa interneti wa 3.75G kwa masaa
25 tangu kujiunga. Kujiunga mteja anatakiwa kupiga *149*99# na
kujichagulia kifurushi kinachomfaa kwa SIKU, WIKI au MWEZI.