Umeonaa! Hivi ni kazi yangu nikimaliza najiajiri. Ndivyo anavyoelekea kusema mwanafunzi Paulina Emmanuel anayejifunza masuala ya ubunifu wa mavazi na mitindo katika chuo cha VETA Chang’ombe Dar es Salaam, akitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa soko la ajira, mipango na maendeleo wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Bw. Enock Kibendela alipotembelea banda a VETA kwenye maonyesho ya SabaSaba, Dar es Salaam.
Mwanafunzi Ernest Maranya wa VETA Chang’ombe akitoa maelezo kwa wageni waliotembelea banda la VETA kwenye maonyesho ya Sabasaba Dar es Salaam akionyesha kifaa cha elimu ya mfumo wa jua na sayansi ya anga jinsi kinavyofanya kazi.
Mkufunzi wa masuala ya hoteli na Utalii katika chuo cha VETA Njiro, mkoani Arusha Theonestina Raphael akitoa maelezo kwa askari polisi waliotembelea banda la VETA kwenye maonyesho ya SabaSaba, Dar es Salaam.
Tukiongeza ufundi kidogo tutakuwa tumemaliza kazi! Ndivyo anavyoonekana kusema Mkurugenzi wa soko la ajira, mipango na maendeleo wa VETA, Bw. Enock Kibendela mwenye kofia alipokuwa akikagua bidhaa za Mamlaka hiyo kwenye maonyesho ya sabasaba, Dar es Salaam.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Mrtibu wa vyuo vya ufundi stadi kanda ya Dar es Salaam Florence Kapinga na Mwenyekiti wa Kamati ya maonyesho Abdul Mollel na Afisa Uhusiano wa VETA Dorah Tesha.
Mafunzo kwa watu wenye mahitaji maalum yanatolewa hivi! Mwalimu Kintu Kilanga mwenye kofia akimueleza Mkurugenzi wa Soka la ajira, mipango na maendeleo wa VETA Bw. Enock Kibendela kuhusu mbinu wanazotumia kumfundisha mwanafunzi Range Jackson (kushoto) mwenye tatizoo la Hyperactive. Hyperactive ni tatizo ambalo linasababisha mtoto kuwa na uelewa dhaifu wa masuala mbalimbali.
Moja ya bidhaa zilizotengenezwa na Range Jackson mwanafunzi wa VETA Chang’ombe anayesoma mafunzo maalum ya uchomeaji.