Mafunzo ya kuwajengea Uelewa Maafisa Habari kutoka katika Wizara zinazohusika moja kwa moja na masuala ya mazingira kuhusu Namna ya Kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi . Vilevile Mpango wa Kupunguza Uzalishaji wa Hewa ya Ukaa kutokana na Ukataji Miti ovyo na Uharibifu wa Mazingira. Mafunzo haya yametolewa na Regalia Media kwa ufadhili wa REDD.
Baadhi ya Maafisa Habari katika mafunzo ya vitendo kuhusu namna ya kupima urefu wa mti ili kuweza kujua kiwango cha kaboni iliyomo katika miti. Zoezi hili limefanyika katika msitu wa kupandwa Morogoro.
Dr. Zahabu akitoa maelekezo ya namna ya zoezi zima la kupima upana wa misitu linavyofanyika.
Washiriki wakijaribu kutumia kipimo kupima kipenyo cha mti katika mafunzo hayo
Picha zote na Asteria Muhozya, Afisa Habari Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto