BONANZA la Maveterani jimbo la Ukonga limefanyika mwishoni mwa wiki na kushuhudia maveterani waalikwa kutoka Sinza timu yenye Star wengi wa zamani ya Golden Bush wakiibuka mabingwa wa mchezo wa Soka.
Bonanza hilo lililoandaliwa na Mbunge wa Jimbo hilo Eugene Mwaiposa lilizikutanisha timu zipatazo kumi za jimbo hilo na timu mbili zilialikwa kwenye Bonanza hilo.
Ushindani kwenye michuano hiyo ulikuwa mkali ambapo wenyeji wa mashindano hayo timu ya Pugu ilitinga fainali na kupambana na timu ya Golden Bush ya Sinza iliyojaza nyota kama Salum Sued Kusi, Abuu Mtiro na Amani Simba.
Hata hivyo haikuwa kazi rahisi kwa mastaa hao kupata ubingwa huo kwa vijana wa pugu hadi pale ilipofikia changamoto ya mikwaju ya Penalt 5, ambapo Golden Bush walipata Penalt saba kwa 6, kutokana na kumaliza muda wote wa mchezo bila kufungana.
Kivutio kikubwa kwenye bonanza hilo kulikuwa kwa mwanamuziki wa kizazi kipya KR Mulla, alipoingia kwa upande wa timu ya Golden Bush na kufanikiwa kuunganisha kross kali na kupiga bao ambapo alishangalia kwa Staili ya mapanga Shaa! na kurusha miguu juu.
Mbunge wa jimbo la Ukonga Eugene Mwaiposa akimkabidhi jezi kapteni wa timu ya vijana wa CCM wa jimbo hilo Abubakari (fulana ya bluu) wakati walipoalikwa kwenye bonanza la maveterani wa jimbo hilo.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga Eugene Mwaiposa akikagua timu za Kigogofresh na Tumaini kabla ya kuanza kwa mpambano wao kwenye bonanza la Maveterani lililoandaliwa na mbunge huyo mwishoni mwa wiki eneo la Pugu Kajiungeni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, matokeo ya mchezo huo Kigogo ilishinda 2 kwa 1.
Wazee wakichuana vikali kumkimbiza kuku.
Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Bombani Pugu akishangilia mara baada ya kukamata kuku aliyeshindaniwa na Wazee wa eneo hilo ikiwa ni miongoni mwa michezo iliyofanyika kwenye bonanza lililoandaliwa na mbunge wa jimbo la Ukonga Eugene Mwaiposa mwishoni mwa wiki.