Mwishoni mwa wiki AAR imetoa huduma ya bure ya mafunzo kwa wafanyakazi wa nyumbani kwa wafanyakazi wa CRDB . Programu hii iliandaliwa na kutolewa na idara ya huduma ya washauri wa kampuni ya bima ya Afya ya AAR (AAR Employees Wellness Program) kwa nia ya kusaidia vijana hawa kuweza kujitambua, kujithamini na kufahamu jinsi ya kumudu majukumu yao kwa vizuri wanayopewa na waajiri wao.
“Tunawashukuru sana AAR kwa kutoa huduma hii kwa wahudumu wetu wa nyumbani, kwani vijana hawa ndio wana muda mwingi wa kukaa na nyumba pamoja na malezi ya watoto wetu kwa muda wote tunapokua kazini , natumai mafunzo haya yatakua na faida kwao na sisi pia kuwa na imani hata tuwapo makazini”. Alisema Meneja Mafunzo wa CRDB, Agnes Robert.
Mafunzo haya yalihusika na mambo mengi mbalimbali, baadhi ikiwa ni pamoja na kujitambua na kujithamini, heshima nyumbani, jinsi ya kulea watoto kiuangalifu na kuwahudumia endapo wapatapo matatizo ya kiafya na mengineyo, vitu muhimu vya kuzingatia ndani ya nyumba ,Vitu visivyopaswa kufatwa.
“Kwakweli leo tumefurahi sana kuja hapa CRDB nakupewa mafunzo na kampuni ya AAR , kwanza kabsa tumepanuka kimawazo, mambo mengi tulikua hatuyajui, na mengine hatukua tunadhani yana umuhimu lakini leo tunashukuru AAR kwa kutusaidia kuyaelewa na pia kujithamini, kujikubali na kupenda kazi zetu..." alisema mmoja kati ya wafanyakazi wa nyumbani hao, Mariam Kayege.
Programu hii inategemea kufanyika tena kwa mara nyingine kwenye makao makuu ya CRDB, na hapo baadae pia kwa makampuni na mashirika mengine mbali mbali nchini.
Wakufunzi wa AAR wakiwa na wafanyakazi wa ndani wa ndani kabla ya kuanza darasa
Mkufunzi wa AAR Josephine Tesha akitoa somo
Bw John Ngonyani AAR akitoa somo
Dkt Kissah wa AAR akitoa mafunzo kwa mifano halisi
Wafanyakazi wa ndani waliohudhuria mafunzo hayo ya AAR
Dr. Kissah wa AAR akiwapa somo wafanyakazi wa ndani namna ya kuhudumia watoto