Dkt Frateline Mlashani Kashaga wa Helsinki, Finland, ni mdau wa siku nyingi wa blog ya jamii katika nchi hiyo ambayo Globu ya Jamii ilizaliwa mwaka 2005. Tangia April, 2008 mpaka mwaka huu 2013 amekuwa kwenye masomo ya PhD in Social Policy , University of Helsinki, Finland . Juzi tarehe 20th June, 2013 aliweza kutetea andiko lake la PhD public defense katika Ukumbi wa Auditorium XII Main Building of the University of Helsinki. Globu ya Jamii inampongeza kwa fanaka hiyo. HONGERA SANA SANA!
Picha ya kwanza, ni Mdau wa Helsinki, Mr. Dennis Londo akimpongeza Dr. Frateline Kashaga mara baada ya kumaliza kutetea nondozzz yake ya PhD katika ukumbi wa chuo kikuu cha Helsinki Finland.
Mdau FRATELINE MLASHANI KASHAGA (PhD) akipongezwa na mai waifu wake kwenye ukumbi wa chuo kikuu cha Helsinki Finland.