Madini ya vito aina ya Tanzanite yanayopatikana na kuchimbwa Tanzania pekee duniani hapa yamekuwa kivutio kwa wananchi katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma-Afrika yanayoaendelea jijini Accra-Ghana.
Wananchi wengi waliotembelea banda la Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) wameeleza kuwa pamoja na kuyaona madini hayo sehemu mbalimbali duniani lakini walikuwa hawana ufahamu wa kutosha kuwa ni Tanzania pekee ndiyo yenye hazina ya madini hayo.
Msemaji wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) Eng. Yisambi E.Shiwa ameeleza kuwa maonesho yamekuwa yakitumika kama nyenzo ya kutoa elimu kuhusu uendelezaji wa sekta ya madini Tanzania ili kuweza kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya Tanzania kuwekeza kwenye rasimali hiyo.
Kamishina wa Tume ya Utumishi wa Umma Ghana Bw.Robertson Akwei Allotey akiangalia madini ya tanzanite yanayoonyeshwa katika banda la Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) jijini Accra
Wananchi wa Ghana wakiwa kwenye banda la Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) ili kupata elimu kuhusu sekta ya madini Tanzania jijini Accra