Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) na Mkewe Mama Mwanamwema Shein (kushoto) pamoja na Mshauri wa Rais Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Uchumi pia Mwenyekiti wa Kamati ya Uchangiaji Vifaa vya Michezo katika Skuli za Serikali za Zanzibar Mhe.Mohamed Ramia wakiangalia picha ya zamani wakati Dk.Shein alivyokuwa akishiriki mchezo wa Riadha katika Skuli ya Lumumba picha hiyo iliyofikishwa katika hafla ya uchangiaji wa Vifaa vya michezo katika Skuli za Serikali za Zanzibar iliyofanyika jana katika viwanja vya Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi Mmoja Mjini Unguja.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein (katikati) wakiwa na Viongozi mbali mbali katika hafla ya uchangiaji wa Vifaa vya michezo katika Skuli za Serikali za Zanzibar iliyofanyika jana katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi Mmoja Mjini Unguja akiwepo Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi (wa pili kulia),[Picha na Ikulu.] 20/05/2017.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Riziki Pembe Juma alipokuwa akitangaza mchango wake wa Milioni moja kumdhamini Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika hafla ya uchangiaji wa Vifaa vya michezo katika Skuli za Serikali za Zanzibar iliyofanyika jana katika viwanja vya Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi Mmoja Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 20/05/2017.

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein alipokuwa akitangaza mchango wa Millioni nane kwa niaba ya familia yake kumdhamini Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa mgeni rasmi katika hafla ya uchangiaji wa Vifaa vya michezo katika Skuli za Serikali za Zanzibar iliyofanyika jana katika viwanja vya Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi Mmoja Mjini Unguja.

Picha ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipiga mpira wakati wa Uzinduzi wa Mashindano ya Vyuo Vikuu ikinadisha wakati wa hafla ya uchangiaji wa Vifaa vya michezo katika Skuli za Serikali za Zanzibar iliyofanyika jana katika viwanja vya Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi Mmoja Mjini Unguja.

Viongozi na Wafanyabiashara mbali mbali wakiwa katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi Mmoja Mjini Unguja wakiwa hafla ya uchangiaji wa Vifaa vya michezo katika Skuli za Serikali za Zanzibar iliyofanyika jana katika mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),[Picha na Ikulu.] 20/05/2017.