Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Dodoma
Tafiti mpya iliyozinduliwa leo inasema serikali inapoteza fedha zaidi ya Sh trillion 4 kwa mwaka kutokana na misamaha na ukwepaji wa kodi.
Pia repoti inasema serikali inasema serikali inapoteza Dola za kimarekani 1.3 biloni (2.9 trilion) kutokana na rushwa na ufisadi katika bajeti ya Taifa.
Hayo yamesemwa na Profesa Honest Ngowi alipokuwa akiwasilisha matokeo ya utafiti na mapitio ya ripoti ya swali la dola bilioni moja na kuja na swali Tanzania inapoteza kiasi gani cha fedha?.
Profesa Ngowi katika mapitio hayo amepata kutaja kuwa , Mfumo wa ulipaji kodi , Mlipa kodi,Misamaha ya kodi ,Utroshwaji wa fedha nje ya nchi na upotevu wa mapato,Ukwepaji kodi, Madhara na Gharama za upotevu na kutokusanywa kodi ipasavyo ni moja ya mambo yanayochangia kupotea kwa fedha hii.
“Tatizo la utoroshwaji wa fedha nje ya nchi na upotevu wa mapato limeangaliwa upya katika utafiti huu na kubaini kuwa Tanzania bado inapoteza mapato kwa njia ya utoroshaji fedha zilizopatikana kwa njia zisizo halali ,Zinaondoshwa nchini visivyo na kutumiwa isivyo halali” amesema Prof Ngowi.
Ametaja kuwa fedha hizo zinaweza kuwa ni fedha zitokanazo na biashara haramu kama biashara ya kulevya , biashara haramu mipakani ,uharamia ,usafirishaji binadamu ,mapato kutokana na ukwepaji kodi na mapato yatokanayo na rushwa.
Kamati ya Viongozi wa dini ya Masuala ya haki za Binadamu ,Kiuchumi na uadilifu katika Uumbaji wakizindua Mapitio ya Ripoti ya Swali la Dola Bilioni moja ,Tanzania inaendelea kupoteza fedha kiasi gani? wakizindua Ripoti hiyo, wakiwa na Wabunge
Kamati ya Viongozi wa dini ya Masuala ya haki za Binadamu ,Kiuchumi na uadilifu katika Uumbaji wakizindua Mapitio ya Ripoti ya Swali la Dola Bilioni moja ,Tanzania inaendelea kupoteza fedha kiasi gani? wakiwa na wabunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakionyesha Vitabu juu mara baada ya uzinduzi.