Na Richard Mwaikenda, Mtama.
WALIMU na Wanafunzi Mkoa wa Lindi, wamefurahishwa na Kampeni ya Kitaifa ya Hedhi Salama kwa Wasichana iliyofanyika kwa uwazi katika Shule ya Sekondari Mtama.
Kampeni hiyo iliyozinduliwa juzi na Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), mjini Lindi, yalishirikisha wanafunzi kutoka shule mbalimbali za msingi na sekondari pamoja na walimu katika Jimbo la Mtama.
Akielezea kuhusu kampeni hiyo, Mwanafunzi Fasda Mahamudu wa Shule ya Sekondari Mtama, alisema kuwa mafunzo aliyoyapata yamemfanya aelewe vizuri kuhesabu siku zake za hevi na jinsi ya kuwa msafi ikiwemo kuoga mara tatu kwa siku na kila baada ya kupata haja.
Naye Amana Amah mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Likongopele, alisema amefurahishwa na kampeni hiyo iliyoendeshwa kwa njia ya uwazi na kwamba imemfumbua mambo mengi ikiwemo kuzijua aina mbalimbali za pad za kisasa na jinsi ya kuzivaa wakati wa hedhi. Aliomba TGGA kuieneza kwa uwazi elimu hiyo katika shule mbalimbali vijijini.
Naye Mratibu Elimu Kata ya Mtama, Marcelinus Lukanga, aliwataka wasichana kujiunga kwa wingi TGGA ili waondokane na woga, hofu na kutokuwa na aibu jambo ambalo pia litawasaidia kuwa huru, safi, salama na kutopata kirahisi maambukizi hasa wakati wa hedhi.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), Mkoa wa Lindi, Sharifa Mkwango akitoa elimu kwa wanafunzi kuhusu Hedhi salama kwa wasichana (Manustretion Hygiene) wakati wa kampeni iliyoendeshwa na chama hicho katika Shule ya Sekondari Mtama, Lindi Vijijini juzi. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA-KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Mwenyekiti wa TGGA Mkoa wa Lindi, Zuhura Mohamed akimkabidhi zawadi ya pad Mkuu wa Shule ya Sekondari Mtama, Asha Namjupa.
Mratibu Elimu Kata ya Majengo, Marsenus Lukanga (kulia) akimkabidhi kasha la vihifadhi (Pad), Mwanafunzi wakati wa Kampeni ya Kitaifa ya Hedhi Salama (Manustretion Hygiene) kwa Wasichana iliyoendeshwa na Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), katika Shule ya Sekondari Mtama, Lindi Vijijini juzi.
Wanafunzi wakishangilia baada ya kufurahishwa na elimu ya hedhi salama.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA