Rais wa Uchezaji wa Mpira wa Miguu Tanzania ‘Free Style Football’ , Morison Jumanne (wakwanza kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maonesho ya kimataifa ya uchezaji wa mpira wa miguu unaonza leo katika maeneo mbalimbali ya wazi na mitaa jijini Dar es Salaam, katikati ni Makamu wa Rais wa Uchezaji wa Mpira wa Miguu Tanzania, Pascal Changa na kushoto ni Bingwa wa Dunia wa Uchezaji wa Mpira wa Miguu 2012 kutoka nchi ya Japan ,Kotaro Tokuda
Bingwa wa Dunia wa Uchezaji wa Mpira wa Miguu 2012 kutoka nchi ya Japan ,Kotaro Tokuda akizungumza na waandishi wa habari juu ya ziara yake nchini Tanzania ni kwa ajili ya maonesho ya wazi ya mchezo huo Mkoa wa Dar es Salaam.
Bingwa wa Dunia wa Uchezaji wa Mpira wa Miguu 2012 kutoka nchi ya Japan, Kotaro Tokuda akionyesha umahiri wa mchezo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.