Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) anaeziwakilisha nchi 23 za Afrika, Bw. Maxwell Mkwezalamba ( kulia) wakipeana mkono baada ya kumalizika kwa Mkutano kati yao uliohusu suala la Uchumi katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia) na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang (kushoto) wakiagana baada ya kumaliza mkutano kati yao, katika Mkutano huo Zhang aliipongeza Serikali kwa hatua nzuri za ukuaji wa Uchumi.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu (kulia) akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) anaeziwakilisha nchi 23 za Afrika, Bw. Maxwell Mkwezalamba (kushoto) baada ya kumalizika kwa Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es salaam
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto) akipongezana na Balozi wa Hungary hapa nchini mwenye makazi yake Nairobi Kenya, Laszlo Mathe (kulia), baada ya kumalizika kwa Mkutano kati yao kuhusu uwekezaji wenye tija kwa pande zote mbili. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA