Yara Tanzania Ltd, imewekeza katika maabara ya kupima udongo ili kuweza kutambua virutubisho vilivyopo na vinavyokosekana kwenye udogo. Mara baada ya matokeo ya udongo kampuni hiyo kupitia wataalamu wake walio bobea kwenye sekta hiyo, hutoa ushauri kwa wakulima nini cha kufanya kulingana na zao lililolimwa au linalotarajiwa kulimwa.
Afisa ugani wa kampuni hiyo Bw. Maulid Mkima, alisema "lengo kuu la kampuni ya Yara Tanzania kuweka maabara ya udongo,ni kuweza kuwapa wateja wao huduma nzuri na mpangilio sahihi wa lishe bora na linganifu ya mimea".