Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 117285

DKT.MABODI: VIONGOZI WA CCM KUFANYENI KAZI ZA KIJAMII

$
0
0

NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

WANANCHI visiwani vya Zanzibar wameshauriwa kuendeleza kwa vitendo Utamaduni wa uzalendo wa kusaidiana wakati wa maafa mbali mbali yanayotokea nchini bila kujadili tofauti za kisiasa na kidini.

Wito huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdalla Juma Saadala “ Mabodi” mara baada ya ujenzi wa nyumba ya Balozi wa Nyumba kumi Bi. Asha Abdalla Baruti iliyobomoka kutokana na maafa ya mvua zinazonyesha nchini, huko Fuoni Migombani.

Dkt. Mabodi alisema maafa yanapotokea hayachagui sehemu ya kuathiri bali yanawakumba wananchi wote hivyo ni muhimu wanajamii kushirikiana kwa mambo ya kijamii na kimaendeleo na kuacha siasa za utengano na chuki.

Ujenzi huo umefanyika kutokana na agizo la Naibu Katibu Mkuu huyo alipowataka uongozi wa CCM na UVCCM Wilaya ya Dimani Unguja, kumjengea makaazi ya muda mwananchi huyo ambaye hakuwa na sehemu ya kuishi kutokana na nyumba yake kuharibiwa na mvua zilizonyesha hivi karibuni.

Alisema hatua ya Chama hicho kutoa msaada na kushiriki katika masuala ya shughuli za kijamii kwa wananchi itakuwa ni utamaduni endelevu kwa Unguja na Pemba.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Abdalla Juma Saadala “ Mabodi” na kushoto ni Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Nd. Abdulghafar Idrissa akifanya kazi ya kukandika udongo katika nyumba ya mwananchi Bi. Asha Abdalla wa Shehia ya Fuoni Migombani aliyebomokewa nyumba yake kutokana na maafa ya mvua zilizonyesha juzi Unguja.
Baadhi ya wananchi wakiwa katika harakati za ujenzi wa nyumba hiyo uko Fuoni Migombani Unguja.
Baadhi ya wananchi wakiwa katika harakati za ujenzi wa nyumba hiyo uko Fuoni Migombani Unguja.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Abdalla Juma Saadala “ Mabodi” akitoa shukrani zake kwa wananchi mbali mbali walioshiriki katika ujenzi huo na kuhakikisha Bi.Asha Abdalla anapata makaazi ya kuishi. Picha na Afisi Kuu CCM Zanzibar.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 117285

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>