Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 117285

Ziara ya Rais wa Zanzibar Dk.Shein kukagua Maeneo yaliyokumbwa na Mafuriko leo

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa tatu kushoto) alipokuwa akiangalia maji ya Mvua yaliyofurika katika bonde la Mwanakwerekwe nyumba mbili leo kutokana na ujenzi holela wa Nyumba za Wananchi zilizojengwa na kupelekea kutopitisha maji katika njia inayoelekea Ziwa Maboga, kutokana na mvua kubwa za Masika zinazoendelea kunyesha.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) alipokuwa akiangalia maji yanayopita katika barabara ya Mwera gudini – Fuoni meli saba leo wakati alipokuwa katika ziara ya kutembelea maoneo mbali mbali yaliyopatwa na maafa ya Mvua za masika zinazoendelea kunyesha (katikati) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe,Ayoub Mohamed Mahmoud.
Pichani ni maji ya Mvua yakiwa yamefurika na kupelekea kufunga njia ambapo wananchi na magari hupita kwa taabu kubwa katika barabara ya Bonde la Kibonde Mzungu,wakati leo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ( hayupo pichani) alitembelea eneo hilo akiwa na ujumbe wake katika ziara maalum
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akitoa maelekezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji Nd,Mustafa Aboud Jumbe (kulia) alipotembelea barabara ya Mwera gudini – Fuoni meli saba leo wakati alipokuwa katika ziara ya kutembelea maoneo mbali mbali yaliyopatwa na maafa ya Mvua za masika zinazoendelea kunyesha (kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe,Ayoub Mohamed Mahmoud.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati)alipokuwa akiangalia ramani inayoonesha utaratibu wa Ujenzi wa Mitaro kutoka kwa Mkuu ya Idara ya Mipango Miji,Kazi na Ujenzi katika Baraza la Manispaa ya Zanzibar Nd,Mzee Khamis Juma (kulia) wakati alipotembelea Bonde la Maji mwanakwerekwe leo akiwa katika ziara maalum ya kutembelea maoneo mbali mbali yaliyopatwa na maafa ya Mvua za masika zinazoendelea kunyesha (kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe,Mohamed Aboud Mohammed. Picha na Ikulu. 14/05/2017.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 117285

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>