Na Humphrey Shao ,Globu ya Jamii
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto amewaomba Vijana wa Temeke kuchangamkia fursa ya Mikopo ya Vijana inayotolewa na Halmashauri hiyo.
Kumbilamoto ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaama alipokuwa akizindua Tamasha la Miaka tisa ya mbio za pole (Jogging) kwa vijana wa Dovya.
"Nawashukuru sana vijana wa Dovya Jogging ya Temeke leo kwa kunialika katika tamasha hili kubwa la kutimiza miaka 9 ya jogging yenu pia kwa upekee nimshukuru Mbunge wa Temeke mh Mtolea kwa kunikaribisha katika jimbo lake nishiriki michezo kwani Muchezo ni ajira hivyo nawaomba mtumie fursa hii kuwaambia mchangamkie fursa za mikopo ya halmashauri ya Temeke inayotolewa kwa Vijana"amesema Kumbilamoto.
Amesema kuwa mikopo hiyo ambayo inatokana na 10% ya mapato ya Halmashauri itawasaidia kujikwamua kiuchumi kama watabuni miradi na kujikusanya katika vikundi .
Amesisitiza hakuna mtu wakuwafata vijana na kuwajaza mapesa mfukoni bila ya wao kujishughulisha katika ujasiliamali na kujiajiri kupitia fursa zinazo patikana .
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akizungumza na Vijana Yombo Dovya wakati wa Tamasha la Michezo la Jonging ya Dovya