Mashindano ya Miss Ustawi wa Jamii 2017 yanatarajia kufanyika siku ya ijumaa, Mei 19 katika Ukumbi wa King Solomon jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mwalimu wa Warembo hao, Clara Nyaki amesema maandalizi yafanyika kwa ustadi kutokana jinsi walivyowachuja. Amesema kuwa mshindi atakayepatikana atakuwa ameonyesha uwezo wake binafsi ikilinganishwa wengine wataofuata.
Clara amesema siku hiyo itakuwa ya kipekee kutokana na maandalizi watapopata mshindi wa kuwakilisha warembo wenzake. Pia, Clara amewakaribisha Watanzania wote kwa ujumla kuja kushuduhia tukio hilo.

Kwa upande wao hao Walimbwende hao wamesema wamejinada kila mmoja kuondoka na ushindi kulingana na maandalizi waliyoyafanya katika kipindi chote walichokuwa na mwalimu wao. Warembo watakaojimwaga siku hiyo ni Ruth Deouratius ,Melody Thomas, Elizabeth Julius, Careen Kileo, Loyce Jeck ,Diana Wambura , Angela Milanzi pamoja na Elice Mwakajila .
Warembo wakiwa katika picha ya pamoja kwa pozi mbalimbali watavyokwenda katika kinyanganyilo hicho kitachofanyika Mei 19 katika ukumbi wa King Solomon jijini Dar es Salaam.