Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 117260

WMA REKEBISHENI MIZANI KWENYE MAGHALA YA KOROSHO-MAJALIWA

$
0
0
*Serikali kugawa salpha bure kwa wakulima wa korosho

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi wa Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) kuhakikisha wanafanya marekebisho ya mizani katika maghala ya kuhifadhia korosho ili kuepuka changamoto ya kutofautiana kwa uzito wa bidhaa hiyo kila inapofikishwa kutoka katika vyama vya msingi.

Amesema kitendo cha mizani za kwenye maghala hayo kupunguza uzito wa korosho zinazopelekwa kutoka kwenye Chama cha Ushirika cha Msingi (AMCOS) hakivumiliki, hivyo Wakala wa Vipimo ipendekeze aina ya mizani zitakazotumika katika upimaji wa korosho.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Mei 13, 2017) wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wadau wa Tasnia ya Korosho uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma.

“Kuna jambo baya sana linaendelea kila korosho inayofikishwa katika ghala kuu lazima kilo ziwe zimepungua kwa zaidi ya kilo mia moja mpaka elfu, kwa nini korosho tani kumi zikiletwa kwenye mizani yenu zinasoma tani nane kwa nini?

“Na huwa haitokei ikasoma tani kumi na mbili, wakati wote huwa inasoma chini tu, watu wa WMA mpo fanyesni marekebisho, haiwezekani tukavumilia wizi huu. Huna mkorosho hata mmoja lakini mwaka huu utasikia umeuza tani zaidi ya elfu tano.Jambo hili lisijitokeze tena,” amesisitiza.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wawa Dau wa Tansnia ya Korosho Nchini ambao umefunguliwa na Waziri Mkuu May 13, 2017 katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango Mkoani Dododma .(PICHA NA OWM)
Wadau wa Tasnia ya Korosho wakimsikilza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wawa Dau wa Tansnia ya Korosho Nchini ambao umefunguliwa na Waziri Mkuu May 13, 2017 katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango Mkoani Dododma
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho , Mama Anna Abdala baada ya Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wawa Dau wa Tansnia ya Korosho Nchini katikati ni Waziri wa Kilimo ,Mifugo na Uvuvi Dr Chales Chizeba , Waziri Kuu amefungua Mkutano huo May 13, 2017 katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango Mkoani Dododma.
(PICHA NA OWM).

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Viewing all articles
Browse latest Browse all 117260

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>