Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 117222

Mradi wa Hakuna Wasichoweza wazidi kuleta faraja kwa watoto wa kike mkoani Lindi

$
0
0
Mradi wa “Hakuna Wasichoweza” unaoendeshwa kupitia taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation na kutekelezwa kwa ushirikiano wa Shirika lisilo la Kiserikali la T-Marc katika mkoa wa Lindi unazidi kuleta faraja kwa watoto wa kike ambapo kwa mwaka huu wasichana wapato 2,000 tayari  wamenufaika nao.

Mradi huu ni mwendelezo wa program ya Hakuna Wasichoweza uliozinduliwa miaka ya nyuma-Mtwara, umewafikia wanafunzi na walimu 10,000 mashuleni kupatiwa elimu ya afya ya uzazi na huduma ya vifaa vya kujisitiri (pedi) wakati hedhi kwa watoto wa kike.

Akiongea na mtandao huu Meneja ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation,Sandra Oswald alisema tangu mradi huu uanze umekuwa na mafanikio makubwa kwa kufikia idadi kubwa ya walengwa wanaosoma katika shule mbalimbali mkoani Lindi ambapo wameweza kupatiwa elimu kuhusiana na mabadiliko ya miili yao katika mchakato wa makuzi na wamewezeshwa kwa kupatiwa taulo za hedhi, Alisema Oswald.

Naye mmoja wa wanafunzi walionufaika na mradi huu, Riziki Athuman (14) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi ya Tandangongoro akiongea kwa niaba ya wenzake kuwa “Hivi sasa wanaelewa kuhusina na suala zima la hedhi na jinsi ya kukabiliana nalo hususani kujiweka katika hali ya usafi na kutumia taulo za kisasa ambazo zinatuwezesha kuendelea na masomo tofauti na awali ambapo wasichana wenzangu wengi walishindwa kuhudhuria vipindi shuleni wanapokuwa kwenye hedhi kutokana na kutokuwepo na mazingira rafiki.

Suala la hedhi lilikuwa halizungumziwi kabisa tofauti na sasa ambapo linajadiliwa na kutafutiwa suluhisho la kukabiliana na changamoto zake hususan kujenga vyoo na miundombinu ya maji mashuleni ya kuwasaidia watoto wa kike wanapokuwa kwenye hedhi”. Alisema Riziki.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 117222

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>