Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kulia akikiongoza Kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar akiwa Mwenyekiti Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Mohamed Aboud Mohamed.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Nd. Ali Juma Hamad akitoa taarifa ya tathmini ya awali ya athari za mvua za masika zinazoendelea kunyesha maeneo mbali mbali ya Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Kanda ya Zanzibar Nd. Mohamed Khamis Ngwali akitoa tathmini ya hali ya Mvua zinazoendelea kunyesha katika ukanda wa Pwani katika Kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi , Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Nd. Mustafa Aboud Jumbe akitoa ufafanuzi wa hatua zilizochukuliwa na Wizara yake za kurekebisha baadhi ya miundombinu iliyoharibiwa na Mvua za Masika zinazoendelea kunyesha. Picha na – OMPR – ZNZ.