Mgeni rasmi katika mashindano ya ngoma za asili kwa Mkoa wa Tabora Mstahiki Meya wa manispaa ya Tabora Gulamhussein Remtullah akizungumza na wakazi wa Mkoa huo katika mashindano hayo chini ya udhamini wa kampuni ya Bia Tanzania kupitia bia yake ya Balimi Extra , mashindano hayo yamefanyika katika shule ya sekondari Iyungi.tolle
Kushoto meneja wa matukio wa kampuni ya Bia Tanzania - tbl kanda ya ziwa Bwana Erick Mwayela akimkabidhi Meya wa Manispaa ya Tabora Mstahiki Meya Gulamhussein Remtullah kitita cha shilingi laki sita ikiwa ni zawadi ya mshindi wa kwanza wa mashindano ya Ngoma za asili kwa mkoa wa Tabora mashindano hayo yamedhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania kupitia Bia yake ya Balimi Extra kulia aliyevaa fulani ya balimi ni kiongozi wa kundi la Mwenge la manispaa hiyo ambao ndio wameibuka washindi wa shindano hilo.
Meya wa Manispaa ya Tabora katikati Akimkabidhi kiongozi wa kundi la Mwenge fedha tasilimu shilingi laki sita mara baada ya kundi hilo kutangazwa Washindi wa shindano la ngoma za asili kwa mkoa wa Tabora ambalo limefadhiriwa na kampuni ya Bia Tanzania Tbl kupitia Bia yake ya Balimi Extra kulia kwake ni Meneja matukio wa kampuni hiyo kanda ya Ziwa Bw Eric Mwayela.