Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115299

KIKAO CHA 38 CHA MKUTANO WA FAO 15-22 JUNI 2013

$
0
0
Mhe. Eng. Christopher Chiza, Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, leo asubuhi tarehe 18 Juni 2013 ametoa hotuba yake, akijadili hali ya chakula na kilimo duniani katika Kikao cha 38 cha Mkutano wa FAO kinacho endelea tangu tarehe 15 Juni 2013 hadi 22 Juni 2013. Mkutano huu, ambao ndiyo ngazi ya juu ya maamuzi katika shirika hili la Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO), hapo tarehe 21 July 2013 utafanya uchaguzi wa Mwenyekiti mpya wa Baraza la FAO (Independent Chair of the FAO Council - ICC), na Mteule (Nominee) wa Tanzania, Balozi Wilfred Joseph Ngirwa, ndiye mgombea pekee wa nafasi hiyo akiungwa mkono na kundi la Afrika na lile la G77 & China. Uchaguzi huo unafuatia Mhe. Luck Guyau, raia wa Ufaransa, kumaliza muhula wake wa pili, na wa mwisho, wa miaka miwili (biennial) kama taratibu za FAO zinavyotaka. Bolozi Ngirwa alikuwa mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN) ya hapa Roma kwa miaka 6 hadi Machi, 2012 ambapo Balozi wetu nchini Italia, Eng. Dr. James Alex Msekela, alichukua nafasi hiyo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115299

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>