Mkuu wa masoko wa Benk ya TIB Corporate ltd Bi. Theresia Soka akipokea hati ya shukran toka Kwa mgeni rasmi Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akishuhudiwa na Waziri wa Ujenzi na uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, Mwenyekiti wa bodi ya makandarasi Mama Consolata Ngimbwa na msajili mkuu wa bodi ya makandarasi Bw. Reuben Nkori. Hiyo ikiwa ni baada ya kudhamini mkutano mkuu wa mwaka wa Bodi ya Makandarasi unaofanyika katika ukumbi wa Jakaya kikwete convention center mjini Dodoma leo.
TIB corporate ni benki ya biashara inayotoa huduma mbalimbali za kibenki katika sekta mbali mbali. Kupitia benki hiyo, Makandarasi wanapatiwa huduma mbalimbali kama vile project financing, overdraft na bank guarantees, unsecured bid bonds, advance payment guarantees na performance guarantees.