Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 117112

MAVUNDE:VIJANA MILIONI 4 KUNUFAIKA NA MAFUNZO YA VITENDO

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde amesema Vijana zaidi ya Milioni Nne nchini watafikiwa na programu ya mafunzo kwa Vitendo ili waweze kuhimili ushindani pindi wanapohitimu vyuo.

Mavunde amesema hayo leo alipokuwa akizindua programu ya mafunzo kwa vitendo iliyoandaliwa na Chama cha Waajiri nchini (ATE) kwa kushirikiana na Shirika la kazi Duniani (ILO) Kanda ya Afrika Mashariki.

“Kwenye program hii ya miaka mitano tunakwenda kuwafikia vijana Milioni Nne nchini ambapo katika mwaka huu wa fedha 2017/2018 vijana 27,000 watapewa mafunzo kwa vitendo” amesema Mavunde.

Waziri Mavunde amewashukuru ATE kwa kuungana na serikali katika kusaidia vijana wa kitanzania kuingia katika mpango huo ambao unaondoa pingamizi la kuwataka vijana kuwa na uzoefu hili waajiriwe katika taasisi mbalimbali.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa ATE , Almas Maige amesema mpango huo utawasaidia waajiri kupata wafanyakazi ambao wataweza kuwasaidia kwa uzalishaji bila ya kuchukua muda mrefu kujifunza.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Anthony Mavunde akizungumza katika uzinduzi wa mpango wa mafunzo kwa vitendo kutoka Kwa Chama Cha Waajiri nchini ATE kwa kushulikiana na Shirika la Kazi Duniani ILO leojijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Anthony Mavunde akionyesha Vitabu vya programu vya mafunzo kwa vitendo mara baada ya kuzindua programu hiyo katika ukumbi wa Hyatt Kempiski leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Anthony Mavunde akikata utepe kuashiria uzinduzi wa programu ya mafunzo kwa vitendo kutoka kwa Chama cha Waajiri nchini ATE, Kulia kwake ni Mwenyekiti wa ATE nchini , Almas Maige(MB) akishuhudia uzinduzi huo leo jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Anthony Mavunde akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa uzinduzi wa programu ya mafunzo kwa Vitendo kwa Vijana .


Viewing all articles
Browse latest Browse all 117112

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>