Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 117024

Madaktari Hospitali ya BLK India Watembelea Muhimbili leo

$
0
0
Madaktari kutoka Hospitali ya BLK ya nchini India leo wametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa lengo la kuangalia mazingira ya kospitali kama yanaruhusu kuanzishwa huduma za upandikizaji Figo (Renal Transplant).

Pia, madaktari hao wametembelea vyumba vya upasuaji, vyumba vya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU), Maabara Kuu pamoja na Radiolojia.

Daktari Bingwa wa Mfumo wa Mkojo ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Urolojia MNH Dk. Ryuba Nyamsogoro amesema mbali na hilo pia wataalam hao kwa kushirikana na watalaam wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wataendesha kambi ya siku mbili kwa ajili ya kutoa huduma ya upasuaji wa kuunganisha mishipa ya damu kwa wagonjwa wanaosafishwa damu (AV Fistula).

‘‘Leo tutawapitia na kuwandaa wagonjwa wote ambao wanatakiwa kufanyiwa upasuaji ili kesho tufanye shughuli hii,’’ amesema Dk. Nyamsogoro. Kambi hiyo itaanza Mei 03 hadi 04, mwaka huu na wagonjwa kati 20 hadi 30 wantarajiwa kufanyiwa upasuaji huo.
Mkurugenzi wa Utumishi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Makwaia Makani ambaye anamwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Lawrence Museru - kizungumza na madaktari kutoka Hospitali ya BLK ya India wanaohusika na upandikizaji wa figo na wataalamu wengine.
Kutoka kulia ni Daktari Bingwa wa Upasuaji wa mfumo wa Mkojo, Dk Hardev Bhatyal wa Hospitali ya BLK ya nchini India, Mkuu wa Maabara wa BLK, Dk. Anil Handoo na Ofisa uhusiano wa hospitali hiyo, Vigyat Singh wakimsikiliza mkurugenzi wa Utumishi, Makwaia Makani leo.
Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji, Dk Julieth Magandi wa Muhimbili, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi wa MNH, Dk Praxeda Ogweyo, Mkurugenzi wa Uuguzi, Agnes Mtawa wa MNH na Mkuu wa Idara ya Urolojia wa hospitali hiyo, Dk Ryuba Nyamsogoro wakifuatilia mkutano huo leo.
Madaktari na wataalamu wengine wa Hospitali ya BLK kutoka India wakitembelea vyumba vya upasuaji Muhimbili leo.
Madaktari na wataalamu wengine wa Hospitali ya BLK kutoka India na wenzao wa Muhimbili wakimsikiliza Mkuu wa Idara ya Mionzi, Dk Flora Lwakatare (kushoto) wakati walipotembelea idara hiyo leo.
Wageni hao wakiwa katika chumba cha ultrasound hospitali ya Taifa Muhimbili leo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 117024

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>