Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala (mwenye tai yenye rangi ya taifa) akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Uholanzi (NUFFIC) Bwana Freddy Weima aliye kushoto kwa Balozi Kamala. Mwanzo kulia ni Bi Ute Jansen Mkuu wa Kitengo cha Mpango wa Uholanzi wa Kujenga Uwezo wa Vyuo Vikuu(NICHE) na wa pili kulia ni Bi Johanna Van Nieuwenhuizen Mkuu wa Idara ya Utawala ya NUFFIC. Balozi Kamala ameishukuru Uholanzi kwa kubuni na kutekeleza mpango wa kusomesha Watanzania Uholanzi kupitia taasisi ya NUFFIC na ameomba Uholanzi kuendelea kutekeleza mpango huo. Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya NUFFIC amebainisha kwamba Serikali ya Uholanzi imeongeza miaka minne kuanzia tarehe moja mwezi ujao kuendelea kusomesha Watanzania Uholanzi katika vyuo mbalimbali. Balozi Kamala ameishukuru serikali ya Uholanzi kwa uamuzi huo. Balozi Kamala amekutana na viongozi wa taasisi ya NUFFIC leo hii ofisini kwao, The Hague, Uholanzi.
↧