Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115292

UBALOZI WA TANZANIA WATANGAZA UTALII WA TANZANIA KWENYE USIKU WA SAN DIEGO ZOO

$
0
0
Kwa mara ya kwanza Tanzania imeshiriki kwenye usiku wa San Diego Zoo, Jimboni California kwa kutangaza utalii wa wanyama Tanzania na vitutio vyake tarehe 15 Juni 2013.

Tanzania iliwakilishwa na Balozi wake wa Hiari kutoka jiji la San Francisco, CA Bw. Ahmed Issa na Afisa Ubalozi Mindi Kasiga ambapo walipata fursa ya kuzungumzia utalii wa Tanzania kwa wageni waliohudhuria na pia kuendeleza mahusiano baina ya San Diego Zoo na Tanzania hususan kwenye upande wa uhifadhi.

Tamasha hili ambalo hufanyika kila mwaka huvutia maelfu ya wadau na washirika wa sekta ya wanyama na utalii wa Marekani na wengi wao hutokea Jimbo la California na vitongoji vyake.

Mwaka huu 2013, ubalozi ulipata mwaliko kutoka kwa mmoja wapo wa waandaji wa tamasha hilo Bw. Richard Rovsek kwa kupitia taasisi yake ya Spirit of Liberty, ambaye alishirikisha (kwa mialiko) baadhi ya nchi ambazo zinatangaza utalii wa wanyama Tanzania, South Africa, Botswana na Kenya.

San Diego Zoo ni mojawapo ya bustani za wanyama kubwa nchini Marekani ambapo ina ukubwa wa hekari za eneo (acres) mia moja (40ha) na inahifadhi aina (species) mia nane za wanyama wapatao elfu nne.

Bustani hii ambayo inashika nafasi ya sita duniani kwa ukubwa wake huandaa tamasha hili maalum kila mwaka ikizawadia washirika wake na kuchangisha pesa kwa ajili ya kuendeshea shughuli zake hususan zile za uhifadhi na elimu kwa umma.

Kwa mwaka 2012 bustani hii ya wanyama iliingiza kiasi cha dola za kimarekani milioni mia saba kwenye uchumi wa Jiji la San Diego ambapo nusu ya gharama hizo ni kutokana na viingilio vya wageni wanaomiminika kila siku.



Mbali na mualiko wa tamasha la San Diego Zoo, Bw. Rovsek aliandaa hafla ya chakula cha mchana kwa heshima ya Mabalozi wa Hiari wa Tanzania, Botswana na Afrika ya Kusini iliyofanyika San Diego Yatch Club nje kidogo ya jiji hilo.
Balozi wa Hiari wa Tanzania Bw. Ahmed Issa akijitambulisha kwenye hafla fupi iliyoandaliwa kwa heshima yake na mabalozi wengine wa hiari watatu na Bw. Richard Rovsek wa taasisi ya Spirit of Liberty mjini San Diego CA tarehe 15 Juni 2013
Bw. Ahmed Issa kwenye picha ya pamoja na Afisa Ubalozi Mindi Kasiga na Bwana na Bibi Richard and Jerry Rovsek baada ya chakula cha mchana na kumtambulisha Bw. Ahmed kwa washiriki wa biashara na wadau wa utalii jijini San Diego, CA.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 115292

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>