Hivi karibuni Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza Dkt Asha Rose Migiro alifanya ziara mjini Leicester ambapo alikutana na Diaspora wa Tanzania waishio katika mji huo na vitongoji pamoja na kujionea shughuli za kiuchumi na kimaendeleo zinazofanywa na Diaspora hao.
Katika mazungumzo yake na Diaspora Balozi Migiro aliwakumbusha dhamira ya dhati ya Rais John Pombe Magufuli na Serikali yake katika Kuwashirikisha Diaspora katika agenda ya Maendeleo ya Serikali na Nchi kwa ujumla. Aidha aliwakumbusha kuwa pamoja na shughuli zao ughaibuni ni Vyema wasisahau kuendeleza nyumbani.
Balozi pia alitumia fursa hiyo kufafanua masuala ya uraia pacha na umiliki wa ardhi kwa Diaspora ambapo aliwaeleza kuwa Sera na Sheria zilizopo ndizo zinazotekelezwa na Serikali katika kuyashughulikia masuala hayo.
Balozi Migiro anatarajiwa kuendelea kuwatembelea Watanzania walio katika miji mingine ya Uingereza kama sehemu ya mpango Kazi wa Ubalozi wa London wa kuwatambua Diaspora wa Tanzania waishio Uingereza na Kuwashirikisha katika Agenda ya Maendeleo ya Serikali ya Awamu ya Tano.
Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza Dkt Asha Rose Migiro akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Diversity Health and Social Care Bi Frida Kusamba kuhusu huduma ya afya inayotolewa na kampuni yake.
Balozi akijionea mavazi yanayoshonwa katika duka la Bi. Farhiya Mayo, Mkurugenzi wa zanzibar fashion house.
Balozi akiongea na wamiliki wa Kampuni ya uandaaji vyakula ya Diaspora Kisk Catering' .
Balozi akijionea mavazi yanayoshonwa katika duka la Bi. Farhiya Mayo, Mkurugenzi wa zanzibar fashion house.
Balozi akiongea na wamiliki wa Kampuni ya uandaaji vyakula ya Diaspora Kisk Catering' .
Balozi katika hali ya kufurahia jambo na Diaspora wa Leicester walioshiriki Mkutano wake