Mjumbe wa kamati ya Utendaji wa Yanga Salum Mkemi (kulia) akiwa sambamba na Katibu Mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Mjumbe wa kamati ya Utendaji wa Yanga, Salum Mkemi ameitwa mbele ya kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kujibu tuhuma zinazomkabili dhidi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPBL).
Kwa mujibu wa barua hiyo, Mkemi anakabiliwa na tuhuma za kuishutumu bodi ya ligi na kuidhalilisha kamati ya utendaji na usimamizi wa kanuni wa ligi (kamati ya saa 72) ya bodi ya ligiu kuwa inaendeshwa kwa unazi na imegubikwa na rushwa katika kushughulikia suala la kadi tatu za njano kwa mchezaji Mohamed Fakhi.
Mbali na kamati, shutuma hizo pia alizielekeza kwa TFF na kuwa na kudai kuwa tayari amesharipoti suala hilo Taasisi ya kuzuaia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU ili kuwachunguza viongozi wa TFF na kamati hiyo.
Kikao hicho kitakachokaliwa siku ya Jumapili kitatoa maamuzi kulingana na utetezi wa Mkemi kutokana na tuhuma zake pia atahitajika kwenda na ushahidi wake atakaouwasilisha mbele ya kamati ya nidhamu.