Maonesho ya wiki ya usalama na afya kazini yameanza leo siku ya Jumatano tarehe 26/04/2017 katika viwanja vya Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro ambapo taasisi mbalimbali za serikali na binafsi zimepata fursa ya kuonyesha namna zinavyozingatia masuala ya usalama na afya kazini kwa wafanyakazi wao.
Miongoni mwa taasisi zilizopata fursa ya kushiriki maonyesho hayo kwa mwaka huu ni pamoja na kampuni za uchimbaji wa madini za Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara ambazo zinamilikiwa na kampuni ya uchimbaji ya Acacia.
Ambapo katika maonesho hayo migodi hiyo ya imekuwa ikionesha vifaa mbalimbali vya uokozi pamoja pamoja na mbinu zitumikazo kuhakikisha mazingira ya usalama kwa wafanyakazi wao wawapo kazini.
Maadhimisho ya mwaka huu ya siku ya afya na usalama mahali pa kazi yameandaliwa na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) yakiwa na kauli mbiu ya “ Ongeza wigo wa ukusanyaji na utumiaji wa takwimu za usalama na afya” .Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufikia kilele chake Aprili 28,2017.
Mkaguzi wa Mitambo Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) kanda ya Kaskazini Boysafi Sabato akifurahia jambo baada ya kufika katika banda la mgodi wa Bulyanhulu
Afisa Mazingira mgodi wa Bulyanhulu Florence Nyuki akimwelezea Mkaguzi wa Mitambo Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) kanda ya Kaskazini Boysafi Sabato namna mgodi huo unavyotunza mazingira na kuhakikisha usalama unakuwepo katika maeneo yao ya kazi
Afisa viwango vya usalama mgodi wa Bulyanhulu Setieli Kimaro akitoa elimu kuhusu mambo ya usalama mgodini kwa wananchi waliotembelea banda la la mgodi wa Bulyanhulu.