Jumanne Aprili 25, 2017 Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Dkt Asha-Rose Migiro, amewaongoza Watanzania waishio Uingereza kushiriki Ibada Maalum ya kuliombea Taifa iliyofanyika katika Kanisa maarufu la Westminster Abbey jijini London.
Ibada hiyo ilifanyika kama sehemu ya kuadhimisha miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Ikiwa mwanachama wa Jumuiya ya Madola, Tanzania hufanyiwa maombi maalum kanisani hapo katika siku hii adhimu kila mwaka.
Pamoja na kusoma maandiko matakatifu, Ibada hiyo ilihusisha maombi maalum kwa ajili ya Mhe. Rais John Pombe Magufuli na Serikali yake, Mahakama na Bunge kama mihimili mikuu ya Amani na Mshikamano wa Taifa la Tanzania na Wananchi wote wa Tanzania ndani na nje ya Nchi.
Ubalozi wa Tanzania London Uingereza unawatakia kheri Watanzania wote waishio Uingereza na Jamhuri ya Ireland katika maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Taifa letu.
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Dkt Asha-Rose Migiro, akiwa amewaongoza Watanzania waishio Uingereza kushiriki Ibada Maalum ya kuliombea Taifa iliyofanyika katika Kanisa maarufu la Westminster Abbey jijini London leo.