Shirika lisilo la kiserikali la APEC limempatia tuzo ya heshima aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam Suleiman Kova katika sherehe za uzinduzi wa chuo jijini Dar es salaam.
Kabla ya kutolewa kwa tuzo hizo, Mkuu wa APEC Bw.Respicius Timanya alitoa wito na kuhamasisha wananchi hasa madereva bodaboda kulaani mauaji ya polisi na kujenga utamaduni wa kuwakinga na majanga kwa kuhakikisha wanatoa taarifa za maovu kwa wakati.
Amesema tukio la mauaji ya polisi lililotokea Aprili 13, mwaka huu,Mkengeni Kata ya Njawa wilaya ya Kibiti mkoani Pwani ni la kulaaniwa na kwamba ana imani halitotokea tena.
Amesema, ana imani kwamba mafunzo hayo ya bodaboda itawawezesha kutambua kuwa ulinzi na usalama ni wajibu wa kila mtanzania hivyo kila mtu mwenye taarifa, tukio ama mtu anayemtilia shaka apeleke taarifa polisi.
Amewaomba waendesha bodaboda 350,000 waliopatiwa mafunzo ya usalama barabarani na Shirika hilo nchini kuzindua kampeni ya kulaani mauji ya polisi na kuhamasisha wananchi kuwa ni wajibu wao kuwakinga.
Kamanda wa Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam Suleiman Kova akiongea machache katika sherehe za uzinduzi wa chuo cha APEC jijini Dar es salaam.
Kamishna wa kazi Hilda Kabisa akiangalia sola ya kuchemshia maji wakati wa uzinduzi wa chuo cha Apec jijini Hapa.
Kamanda mstaafu Suleiman Kova akionesha cheti cha heshima alichopewa na chuo hicho