Wanachama wa chama cha Kariakoo Family Development Foundation (KFDF) wamejipatia uongozi mpya baada ya kufanya mkutano mkuu wa uchaguzi siku ya Jumapili Aprili 23, 2017 katika ukumbi wa shule ya Msingi ya Jamhuri jijini Dar es salaam. Jumla ya wanachama hai na halali 41 walishirki katika uchaguzi huo, ambapo wanachama 23 walikuwepo ukumbini na wanachama 18 waishio nje ya nchi walipiga kura kwa njia ya mtandao.
Bw. Alkarim Bhanji alishinda nafasi ya Uenyekiti akiwa mgombea pekee, wakati Bw. Mohamed Irapo alinyakua nafasi ya Makamu Mwenyekiti. Katibu Mkuu wa kipindi cha mpito Bw. Wahid Abdulghafoor aliweza kutetea kiti chake akiwa mgombea pekee. Nafasi ya Katibu Mkuu msaidizi imechukuliwa na Bw. Fabian Kimongw wakati Bw. Bakari Simba ametetea tena nafasi ya Mweka Hazina Msaidizi aliyokuwa akishika wakati wa kipindi cha mpito.
Katika uchaguzi huo uliokuwa umesimamiwa vyema na Katibu Mkuu wa klabu ya michezo ya Saigon, Bw. Boi Juma, jumla ya wajumbe watano kati ya sita wanaotakiwa kikatiba walichaguliwa. Hao ni Bw. Shaaban Kessy Mtambo, Bw. Abdallah Kizua, Bw. Idrissa Jumbe, Bi. Sophia Muccadam na Bi. Salma King.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa KFDF Bw. Wahid Abdulghafoor, nafasi mbili za Mweka Hazina na Mjumbe mmoja zilizo wazi baada ya kutotokea mgombea zitajazwa baadaye katika uchaguzi mdogo.
KFDF ni chama kinachojumuisha wananchi wanaoishi ama waliopata kuishi eneo lote Kariakoo, dhumuni kuu likiwa ni kuwaunganisha upya na kufanya shughuli za kijamii kimaendeleo kwa lengo la kudumisha na kuendeleza umoja, mshikamano na undugu uliokuwepo miongoni mwa wakaazi wa eneo hilo maarufu la jiji la Dar es salaam toka enzi za mababu.
KFDF ni chama kinachojumuisha wananchi wanaoishi ama waliopata kuishi eneo lote Kariakoo, dhumuni kuu likiwa ni kuwaunganisha upya na kufanya shughuli za kijamii kimaendeleo kwa lengo la kudumisha na kuendeleza umoja, mshikamano na undugu uliokuwepo miongoni mwa wakaazi wa eneo hilo maarufu la jiji la Dar es salaam toka enzi za mababu.
Msimamizi wa uchaguzi Bw. Boi Juma (mwenye bahasha mkononi) akipata picha ya pamoja na safu mpya ya uongozi wa KFDF pamoja na wanachama waliopo nchini baada ya kuhitimisha zoezi hilo siku ya Jumapili Aprili 23, 2017 katika ukumbi wa shule ya Msingi ya Jamhuri jijini Dar es salaam |
Msimamizi wa uchaguzi Bw. Boi Juma (kati) akipata picha ya pamoja na safu mpya ya uongozi wa KFDF siku ya Jumapili Aprili 23, 2017 katika ukumbi wa shule ya Msingi ya Jamhuri jijini Dar es salaam. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA |